Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Shule ya Msingi Iboni ya Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum iliyopo Wilaya ya Kondoa wakati akiwa ziarani mkoani Dodoma tarehe 21 Agosti 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Mji wa Kondoa Said Majaliwa kuhusu ujenzi wa mabweni katika Shule ya Msingi Iboni ya Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum iliyopo Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma tarehe 21 Agosti 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasalimu wanafunzi wenye mahitaji maalum wakati alipotembelea Shule ya Msingi Iboni ya Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum iliyopo Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma tarehe 21 Agosti 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalum mara baada ya kutembelea na kukagua Shule ya Msingi ya Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum ya Iboni iliyopo Wilaya ya Kondoa wakati akiwa ziarani mkoani Dodoma tarehe 21 Agosti 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kondoa mara baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo akiwa ziarani mkoani Dodoma tarehe 21 Agosti 2024.
……….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametoa rai kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kuacha tabia ya kuwaficha na kuwanyima fursa muhimu ya kupata elimu.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kondoa mara baada ya kutembelea shule ya Msingi Iboni inayojumuisha watoto wenye mahitaji maalum akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani humo katika mkoa wa Dodoma.
Amesema licha ya serikali kujenga miundombinu ikiwemo mabweni na madarasa kwaajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum bado idadi ya watoto hao imeendelea kuwa ndogo katika vituo vya kutolea elimu.
Amesema mathalani katika Wilaya hiyo ya Kondoa, watoto 30 pekee wenye mahitaji maalum wamepelekwa katika shule ya Iboni ikiwa shule hiyo inauwezo wa kupokea wanafunzi 200.
Makamu wa Rais amesema kitaaluma watoto wenye mahitaji maalum wana uwezo mkubwa pamoja na vipaji. Amewahimiza viongozi wa serikali, dini, vyama na wananchi kutoa msisitizo wa kuwatafuta watoto wenye mahitaji maalum waliopo majumbani na kuhakikisha wanapelekwa kupata elimu.
Shule ya Iboni inayojumuisha watoto wenye mahitaji maalum imekamilisha mradi wa Ujenzi wa Mabweni Mawilli ambao umegharimu shilingi milioni 270.9. Mradi huo unatarajiwa kuondoa changamoto ya wanafunzi wenye mahitaji maalum kusafiri umbali mrefu wa kutoka nyumbani kwenda shuleni.
Mradi huo pia utapunguza changamoto ya wanafunzi kutokufika shule kwa wakati pamoja na kuchangia kuweka mazingira bora na salama kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Makamu wa Rais anaendelea na ziara ya kikazi ya siku nne katika mkoa wa Dodoma.