Mshauri Elekezi kutoka Wakala wa Majengo Zanzibar Abubakari Mohamed Bakari akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi walipofanya ziara ya kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar Leo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Zanzibar.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita katikati akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar Leo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Zanzibar.
Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Ali Haji Mwadini kulia akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yalioulizwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi wakati walipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar Leo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi wakiangalia ubora wa Ujenzi wakati walipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar Leo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi wakipata maelezo kutoka kwa Mshauri elekezi kutoka wakala wa Majengo Abubakari Mohamed Bakari wakati walipofanya Ziara kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar Leo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Sabiha Filfil Thani akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufanya ziara kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar Leo Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Zanzibar.
……………….
NA ALI ISSA NA NAJJASH UBWA. MAELEZO.
KAMATI YA KUDUMU YA USTAWI WA JAMII KATIKA BARAZA LA WAWAKILISHI IMERIDHISHWA NA UJENZI WA OFISI YA SHIRIKA LA MAGAZETI YA SERIKALI ZANZIBAR IKIWEMO GAZETI LA ZANZIBAR LEO.
HAYO YAMEELEZWA NA MWENYEKITI WA KAMATI HIYO MHE. SABIHA FILFIL THANI WAKATI KAMATI HIYO ILIPOFANYA ZIARA KUANGALIA MRADI WA UJENZI WA OFISI HIYO HUKO TUNGUU WILAYA YA KATI UNGUJA.
AMESEMA HATUA YA UJENZI INARIDHISHA NA KUTIA MOYO JAMBO AMBALO LINALETA MATUMAINI YA UJENZI WAKE KUKAMILIKA KWA MUDA ULIOPANGWA.
AIDHA AMEIOMBA SERIKALI KUZIDI KUTOA USHIRIKIANO NA SHIRIKA HILO ILI KUONA UJENZI HUO UNAFANIKIWA NA KUFIKIA MALENGO YALIOKUSUDIWA.
WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO MHE. TABIA MAULID MWITA AMESEMA KUKAMILIKA KWA UJENZI HUO, UTAONDOA CHANGAMOTO ZINAZOLIKABILI SHIRIKA HILO IKIWEMO UDOGO WA OFISI WANAYOTUMIA KWA SASA NA UKOSEFU WA YA MTAMBO WA KUCHAPISHIA MAGAZETI.
AIDHA MHE. TABIA AMEISHUKURU SERIKALI KWA JUHUDI INAZOZICHUKUWA YA KUHAKIKISHA MIRADI YOTE YA SERIKALI INAMALIZA KWA MUDA ULIOPANGWA.
MAPEMA MSHAURI ELEKEZI KUTOKA WAKALA WA MAJENGO ZANZIBAR ABUBAKAR MOHD BAKARI AMEAHIDI UJEZI HUO KUMALIZIKA MWEZI WA TISA MWAKANI NA TAYARI UMESHAFIKIA ASILIMIA 30.
HATA HIVYO AMESEMA UJEZI HUO, UNATARAJIWA KUGHARIMU KIASI YA SH. BILIONI 8 AMBAO UNAJENGWA NA KAMPUNI YA SKY WARD CONSTRUCTION LIMITED YA ZANZIBAR NA UNATARAJIWA KUWA NA MAJENGO MATANO, IKIWEMO NA NYUMBA ZA WAFANYAKAZI, KIWANDA CHA KUCHAPAJI MAGAZETI NA MSIKITI.