Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ametembelea kuona nakukagua ujenzi wa mradi mkubwa wa bandari ya uvuvi ya kisasa inayojengwa Wilayani kilwa Mkoani Lindi yenye thamani ya Bil 266, na kuridhishwa na hatua ya ujenzi wa bandari hiyo inayojengwa na kampuni ya Chinese Harbour.
Mhe. Telack akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo amesema kuwa kwa hatua ambayo ujenzi umefikia hadi sasa ni wazi kuwa mradi utakamilika kwa wakati ambapo mkataba unaonesha mwisho wa ujenzi ni Februari, 2024.
Kwa upande wake Mkandarasi Msaidizi wa kampuni hiyo Ndugu Aren Kapwa amesema kuwa hadi sasa ujenzi umefikia 72% ikiwa matarajio kufikia 66 hivyo wamevuka lengo, kwani majengo na miundombinu mingine imefikia hatua nzuri .
Mhe. Telack amesisitiza kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia muda na ubora .