Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akioneshwa kifaa maalum cha kutambua ubovu wa gari na Mhandisi wa Mitambo TEMESA Mustapha Abdul, kwenye ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Chama Cha Madereva wa Serikali, uliyofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha Agosti 20, 2024. Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya na Mkurugenzi wa Ufundi na Matengenezo TEMESA Hassan Kalonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akioneshwa vitendea kazi vya ufundi wa magari na Mkurugenzi wa Ufundi na Matengenezo TEMESA Hassan Kalonda, kwenye ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Chama Cha Madereva wa Serikali, uliyofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha Agosti 20, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Meneja Tathmini Vihatarishi Sehemu za Kazi WCF Naanjela Msangi, wakati alipotembelea kwenye ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Chama Cha Madereva wa Serikali, uliyofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha Agosti 20, 2024. Kulia ni Afisa afya na Usalama Mwandamizi Robert Duguza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea tuzo kwa niaba ya Rais kutambua mchango wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya Madereva wa Serikali Tanzania, kwenye ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Chama Cha Madereva wa Serikali, uliyofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha Agosti 20, 2024. Kulia ni Afisa afya na Usalama Mwandamizi Robert Duguza. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya na kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Serikali Taifa Frala Mnyandavile. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwenye ufunguzi wa Kongamano la Tatu la Chama Cha Madereva wa Serikali, lililofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha Agosti 20, 2024. Kulia ni Afisa afya na Usalama Mwandamizi Robert Duguza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)