Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wa maeneo ya jirani na Tasani mara baada ya hafla ya Ufunguzi wa Skuli ya Maandalizi ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makunduchi mkoa wa Kusini Unguja, tarehe 20 Agosti 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano hundi ya Shilingi milioni 63.8 kutoka Asasi ya Sekta Binafsi inayojishughulisha na kuendeleza sekta ya Horticultural Tanzania (TAHA) kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kilimo biashara kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya Tamasha la Kizimkazi iliyofanyika katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 20 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea mfano hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kilimo biashara kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya Tamasha la Kizimkazi katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 20 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwakabidhi vyeti Wahitimu wa mafunzo ya Kilimo Biashara, Ujasiriamali pamoja na Utalii kwenye hafla ya kufunga mafunzo ya Tamasha la Kizimkazi katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 20 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi kabla ya kufunga mafunzo ya Tamasha la Kizimkazi katika uwanja wa Mwehe Makunduchi Kusini Unguja, Zanzibar tarehe 20 Agosti, 2024.