Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiagana na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipokea zawadi ya mfuko wenye kitabu chenye taarifa za ushirikiano wa miaka 60 kati ya Tanzania na Uswisi, wakati wa tukio la kuagana na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot (wa tatu kushoto), katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi. Wengine katika picha kushoto ni Mwambata wa Ubalozi wa Uswisi-Tanzania, Bw. Dany Currat, na Naibu Balozi wa Uswis hapa Nchini, Mhe. Holger Tausch. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Idara ya Fedha za Nje, Bw. Melkizedeck Mbise na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tatu kushoto), akiongoza kikao kati yake na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot, aliyefika kumuaga katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba, aliihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa tatu kulia), akizungumza jambo akiwa na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot, alipofika kumuaga katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Dkt. Nchemba aliihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot (Katikati), akizungumza jambo alipofika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kumuaga Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), ambapo ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa kimaendeleo katika kipindi kifupi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tatu na kuahidi kuwa nchi yake itaendeleza ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), akizungumza jambo wakati akiagana na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati akiagana na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, ambapo ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot. akizungumza jambo alipofika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kumuaga Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), ambapo ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa kimaendeleo katika kipindi kifupi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tatu na kuahidi kuwa nchi yake itaendeleza ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot (Katikati), akizungumza jambo alipofika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, kumuaga Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), ambapo ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa kimaendeleo katika kipindi kifupi cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tatu nakuahidi kuwa nchi yake itaendeleza ushirikiano na Tanzania katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Dar es Salaam)
………
Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali inaendelea kuweka na kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo yake ya kodi.
Dkt. Nchemba ameyasema hayo katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam, wakati akiagana na Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake wa ubalozi hapa nchini, Mhe. Didier Chassot.
Alisema kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameunda timu ya wataalam ya kupitia na kuja na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha mifumo yake ya kodi ili kuvutia zaidi biashara na uwekezaji nchini.
Mhe. Dkt. Nchemba alifafanua kuwa pamoja na kuundwa kwa timu hiyo, Serikali pia imechukua hatua kadhaa za kuboresha ya kielektroniki ya ukusanyaji kodi inayosaidia kukusanya mapato yake kwa ufanisi na kuondoa usumbufu kwa walipa kodi.
Alisema kuwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na kuimarisha mifumo ya kodi ni kuhakikisha kuwa idadi ya walipakodi inaongezeka hatua itakayosaidia pia kuiwezesha Serikali kupunguza viwango vya kodi ya ongezeko la thamani siku za usoni kwa sababi walipakodi watakuwa wengi.
Kwa upande wake Balozi wa Uswisi aliyemaliza muda wake hapa nchini, Mhe. Didier Chassot, aliipongeza Serikali kwa uamuzi huo wa kupitia mifumo ya kodi na kwamba anaamini Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini watapata pia nafasi ya kuzungumza na kujadiliana na Serikali kuhusu masuala hayo kama walivyoomba.
Balozi Chassot alitumia fursa hiyo ya kuagana na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa hatua kubwa iliyopiga kimaendeleo katika kipindi kifupi.
Aliahidi kuwa Uswisi inaandaa mpango mpya wa ushirikiano wa kimaendeleo na Tanzania, utakaojielekeza katika kufanikisha agenda mbalimbali za maendeleo ya nchi kupitia program zake mbalimbali ikiwemo kusaidia mfuko wa maendeleo ya jamii-TASAF, usimamizi wa fedha za umma, biashara na uwekezaji kupitia asasi za kiraina sekta binafsi.
Mhe. Didier Chassot, ameitumikia nafasi hiyo ya ubalozi akiwa hapa nchini kwa kipindi cha miaka minne na ameahidi kuendelea kuwa Balozi mzuri wa Tanzania atakaporejea nchini kwake kuendelea na majukumu yake mengine.