NA BALTAZAR MASHAKA,MWANZA
“Tukio hili ni la kihistoria la kufungua Msikiti huu wa Al-Ghazal Mahina,yalisemwa mengi kuhusu fedha za ujenzi wa msikiti huu lakini leo msikiti umefunguliwa wa kisasa baada ya kuvunjwa wa zamani kupisha mradi wa SGR,”amesema bila kufafanua.
Sheikh Kabeke amewataka wasaidizi wake waendelee na mwendo wa kuziba masikio mithiri ya chura kiziwi ili wawaleletee waislamu maendeleo wana Mwanza kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Sheikh huyo wa Mkoa wa Mwanza,BAKWATA chini ya Mufti Dk.Sheikh Abubakar Bin Zubeir Bin Ally Mbwana ( Mujaddidul asri),inafanya kazi kwa uadilifu uliojaa uaminifu ingawa mapungufu kwa mwanadamu hayakosekani,hivyo jitihada zaidi za kukifanya chombo hicho kiendelee kuwatumikia waislaam zinafanyika.
Aidha Alhaji Kabeke ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita na kummwagia sifa Rais Dk.Samia Suluhu Hassam kwa kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo SGR.