RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa TUZO Maalumu na Mkurugenzi Muendeshaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Arafat Ally Haji, baada ya kulifungua Tamasha la Tisa la Kizimkazi 2024, katika viwanja vya Kizimkazi Mkunguni Wilaya ya Kusini Unguja leo 18-8-2024.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum ya Fulana na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Vijana Nguvu Kazi Ndg. Abuu Sufiani Juma, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Tamasha la Tisa la Kizimkazi 2024, lililozinduliwa leo 18-8-2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, katika viwanja vya Kizimkazi Mkunguni.(Picha na Ikulu)
WANANCHI mbalimbali wakishiriki katika zoezi la kuchangia Damu wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Tamasha la Tisa la Kizimkazi 2024, linalofanyika katika viwanja vya Kizimkazi Mkunguni Wilaya ya Kusini Unguja leo 18-8-2024.(Picha na Ikulu).
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia hutuba ya Ufunguzi wa Tamasha la Tisa la Kizimkazi 2024, katika viwanja vya Kizimkazi Mkunguni Wilaya ya Kusini Unguja, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Tamasha hilo leo 18-8-2024 na (Kushoto kwake) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),Mhe. Mohamed Mchengerwa na (kulia kwake) Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Kizimkazi Ndg. Mahmoud Said Omar.(Picha na Ikulu)