NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwakomboa vijana katika kujikwamua kiuchumi ameahidi kuwasaidia vijana wa kata ya Tangini kuanzisha miradi mbali mbali ikiwemo kuwapatia pikipiki.
Koka ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na vijana wa UVCCM kata ya Tangini wakati kufunga rasmi kikao cha baraza la vijana lenye lengo la kuweza kujadili mambo mbali mbali ikiwemo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
“Kikubwa vijana wa kata ya Tangini mimi Mbunge wenu nipo pamoja nanyi lakini kitu kikubwa inabidi muungane kwa pamoja na mkiwa tayari mimi nitawasaidia katika miradi mbali mbali ikiwemo kuwapatia pikipiki ambayo itawasaidia kuwaingizia kipato,”alisema Koka.
Koka alisema kwamba ataendelea kuwa bega kwa bega na vijana hao wa kata ya Tangini katika kuwasaidia katika nyanja mbali mbali kwa lengo la kuweza kuleta chachu ya kimaendeleo.
Aidha Mbunge huyo amewataka Vijana wa chama Cha mapinduzi UVCCM kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kwamba atakuwa tayari kutoa ushirikiano Kwa kijana ambaye atajitokeza kugombea.
Amesema kwamna atajisikia furaha kubwa kuona vijana nao wanajitokeza kwa wingi kugombea na kuongoza serikali za kitaa na pia kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika mitaa yote.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa vijana Wilaya ya Kibaha mjini(UVCCM)) Ramadhani Kazembe amewataka Vijana kukaa na kuangalia ni kijana gani wanayeweza kumteua ili kugombea nafasi hizo na yeye atakuwa nao bega Kwa bega.