Mkurugenzi wa Mipango kutoka Wizara ya Fedha Moses Dulle (mwenye suti ya kijivu) akizindua Kituo cha Mafunzo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kilichopo katika Kijiji cha Kitumba,Kata ya Kisesa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa Mipango kutoka Wizara ya Fedha Moses Dulle akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa Mwanza cha Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini
Moja ya jengo la Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya ziwa Mwanza cha Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini.
Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo Cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa .
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Kituo cha Mafunzo cha Kanda ya Ziwa Mwanza cha Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini
………….
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Kituo Cha Mafunzo Kanda ya Ziwa kilichopo Jijini Mwanza chini ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kimetakiwa kuongeza jitihada za kufanya tafiti zenye kulenga kuondoa changamoto za kijamii na kiuchumi.
Rai hiyo ilitolewa Jana Jumamosi Agosti 17,2024 na Mkurugenzi wa Mipango kutoka Wizara ya Fedha, Moses Dulle wakati akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo hicho kilichopo Kisesa Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza.
Aidha, amesema matokeo ya tafiti hizo yaandikwe kwa lugha rahisi ya kiswahili ili kila mwananchi anayejua kusoma na kuandika aweze kusoma na kuelewa.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini,Profesa Hozen Mayaya amesema tangu kuanzishwa kwa kituo hicho Septemba 25, 2011 kimeshafanya jumla ya shughuli 20 za tafiti,ushauri na uelekezi kwakushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo likiwemo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambapo shughuli hizo zimesaidia katika juhudi za Serikali za kuwaongezea wananchi kipato na kuwapunguzia umasikini.
Amesema idadi ya wanafunzi waliodahiliwa na kusajiliwa imeongezeka kutoka wanafunzi 323 wanaume wakiwa 164 na wanawake 159 mwaka 2011/12 hadi kufikia wanafunzi 3,845 wanaume wakiwa 1,776 na wanawake 2,069 katika mwaka wa masomo 2023/24.
Naye Mwenyekiti wa Balaza la Uongozi wa Chuo hicho, Profesa Joseph Kuzilwa ameahidi kuitunza miundombinu hiyo vizuri ili itumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kwa muda mrefu.