Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila Chalamila leo Agosti 17, 2024 amezindua mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva wa bodaboda mkoa wa Dar es salaam yanayoendeshwa na kanisa la Arise and Shine chini ya Mchungaji Mwamposa ambapo Mkuu wa Mkoa amelipongeza kanisa hilo na kuwataka viongozi wa dini kuiga mfano huo unaooneshwa na Mchungaji Mwamposa huku akikemea tabia ya kubeza kazi nzuri inayofanya na kanisa la Arise and shine
Mhe Albert Chalamila amewataka viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na Serikali kwenye masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo uwezeshaji kwa vijana ili kuwa na Taifa lenye vijana waadilifu,wachapakazi, wapenda amani na wenye hofu ya Mungu
Aidha Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule amewataka vijana kuendelea kuwa walinzi wa amani ya nchi kwa kuhakikisha hawashiriki kwenye matendo maovu na kufichua wahalifu na kueleza kuwa bodaboda ni kiungo muhimu kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi kwani hurahisisha usafiri
Naye Mwanzilishi wa mashindano hayo ya bodaboda Cup Mchungaji wa makanisa ya Arise and Shine
Mchumgaji Boniface Mwamposa amesema kanisa lake linatambua mchango wa bodaboda katika kusafirisha waumini kwenda kanisani na kwenye shughuli mbalimbali hivyo mashindano hayo ni katika kutambua na kurejesha fadhila kwa madereva wa bodaboda
Hata hivyo Mkurugenzi kituo cha Radio cha Efm na TvE Francis Siza maarufu kama Majizo aliposhiriki uzinduzi huo amesema anatambua umuhimu wa boda boda kama maafisa usafirishaji na amekuwa akishirikiana nao kila siku na kwamba ataendelea kushirikiana nao wakati wote
Mwisho mashindano hayo yaliyoandaliwa na Mchungaji wa Makanisa ya Arise and Shine Boniface Mwamposa yatashirikisha timu 60 kutoka wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es salaam ambapo mshindi wa kwanda atapata bodaboda 5,mshindi wa pili bodaboda 3 na mshindi wa 3 badaboda 2