Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ Troika Summit), Harare nchini Zimbabwe, tarehe 16 Agosti, 2024.
Rais Mhe. Hakainde Hichilema wa Zambia akizungumza kwa njia ya Mtandao katika kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- Organ Troika Summit) jijini Harare Zimbabwe.
………………
NA JOHN BUKUKU – HARARE ZIMBABWE
Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Sululu Hassan Kwa kusimamia Uenyekiti wake alipoongoza kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC- Organ Troika Summit) akimuwakilisha Mwenyekiti wa Asasi hiyo, Rais wa Zambia Hakainde Hichilema.
Akizungumza kwa njia ya mtandao katika Mkutano huo Agosti 16 2024 Mwenyekiti wa Asasi hiyo, Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema Amesema Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameaminiwa Kwa kusimamia uenyekiti wake hata kabla ya kukabidhiwa uongozi kama Mwenyekiti ajaye kwa Kuwa Tanzania imekuwa Mfano Bora hususan katika Demokrasia pamoja na kuaminiwa na Wakuu wa nchi wote wa nchi za SADC.
Mhe. Hichilema ameongeza kwamba yeye mweyewe anamuunga mkono na yuko tayari kumsaidia kwa nguvu zote wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ Troika Summit)
Leo Agosti 17, 2024 katika mkutano wa wakuu wa nchi na viongozi wa serikali wa SADC unaofanyika katika Jengo jipya la Bunge la bunge la Zimbabwe (New Parliament Building) lililoko katika eneo la kilima cha Mount Hapdeo jijini Harare.
Rais Dkt. Samia anatarajiwa kupokea uenyekiti wa SADC Organ Troika katika mkutano huo wa 44 wa SADC Kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo atapokea kutoka kwa Rais Hakainde Hichilema wa Zambia anayemaliza muda wake wa uongozi.