Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Agost 15, 2024 amewasili katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es salaam na kupokelewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel pamoja na Menejimenti na watumishi wa Wizara wakiongozwa na Katibu Mkuu Dkt. John Jingu.
Mhe. Mhagama amewasili katika ofisi hizo mara baada ya kuapishwa Ikulu leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Afya.
Mhe. Mhagama amezungumza na watumishi wa Wizara hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa bidii, weledi na utulivu ili kutafsiri uwekezaji mkubwa uliofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha zaidi ubora wa huduma za Afya.
Nae Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema viongozi waliopita walifanya kazi kubwa na kuifikisha Wizara mahali ilipo sasa na ana imani Wizara hiyo itaendelea kusonga mbele chini ya Rais Samia kupitia uongozi huo mpya kuboresha ubora wa huduma na kusimamia Sekta ya Afya kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Jingu amemkaribisha Waziri Jenista na Kumuahidi ushirikiano katika kuboresha hali ya utoaji wa huduma za Afya nchini.
Waziri Jenista pia ameeambatana na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Afya Eng. Ismail Rumatila na Mtendaji Mkuu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dkt. Irene Isaka ambao wote wameapishwa leo.