RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa KIislamu Tanzania (JUWAKITA), Mkoa wa Mwanza, Amina Masena, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), leo kuhamasisha wasichana wenye uwezo wa kusoma na kuhifadhi Kuran kushiriki mashindano ya kimataifa jijiji Dar es Salaam. Picha na Baltazar Mashaka.
…………
NA BALTAZAR MASHAKA,MWANZA
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya Kimataifa ya Kusoma na Kuhifadhi Kuran yaliyoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
Mashindano hayo yatakayofanyika Agosti 31, mwaka huu,katika Uwanja wa Benjamin Mkapa,yatashirikisha wasichana wa dini
ya kiislamu yakiwa na malengo makubwa matatu.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hasani Kabeke,akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa,jana (leo Agosti 16,2024) aliwataka wazazi
kuwapa watoto wao fursa ya kushiriki mashindano hayo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Dk.Samia.
Amesema mashindano hayo yatakayohudhuriwa na Katibu wa taasisi ya Muslim World League ya ncini Saudi Arabia,Mohamed
Bdulkarim Al-ssa,yanahamasisha usomaji wa Kuran na kuingiza upendo wa Kuran hiyo tukufu katika nyoyo ikiwa ni pamoja na kuihifadhi.
Sheikh Kabeke amesema pia ni kuwaenzi wote waliotoa mchango mkubwa katika kuisoma Kuran na
kuihifadhi, waliotangulia mbele ya haki.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa dini utazinduliwa mradi wa kurekodi Msahafu kwa Qira’at zote kumi ikiwa ni hatua
kubwa ya kuongeza ufahamu,upatikanaji wa usomaji sahihi wa Kuran tukufu.
“Uongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza,unaawalika waislamu na wasio waislamu kuhudhuria na kushuhudia mashindano hayo bila
kukosa hasa viongozi wote wa taasisi hiyo ya dini kuanzi ngazi ya msikiti hadi mkoa,”amesema
Sheikh Kabeke ameeleza ili kurahisisha usafiri wa washiriki na wengine kwenda jijini Dar es Salaam,uongozi wa BAKWATA
Mkoa wa Mwanza,umeweka utaratibu na unaratibu usafiri wa pamoja.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA) Mkoa wa Mwanza,Amina Masenza,amesema mashindano hayo ya kusoma na kuhifadhi Kuran ni fursa,inarithisha kizazi hadi kingine na hivyo wasichana wenye uwezo wakashiriki kwa sababu yanatia hamasa kwa wasikilizaji.
“Ni jambo la kufurahisha sisi wasikilizaji,washiriki watajifunza na kuja kufundisha namna bora ya kughani Kuran na
taratibu zake,rai yangu kwa wazazi wenye watoto wa kike wawape fursa wakashiriki mashindano
hayo,”amehimiza.