NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umetoa msaada wa shilingi
milioni 10 kwa lengo la kuboresha huduma za afya nchini, kupitia mbio za CRDB
Marathon.
Akikabidhi
msaada huo Agosti 16, 2024 kwenye Makao Makuu ndogo ya PSSSF jijini Dar Es
Salaam, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Bw. Yesaya Mwakifulefule amesema,
PSSSF imeungana na CRDB ili kusaidia juhudi za serikali za kuboresha huduma za
afya na hivyo kusambaza tabasamu kwa wenye uhitaji na jamii nchini, ambapo
fedha zitakazopatikana zitakwenda kuwasaidia watoto wenye maradhi ya moyo na
akina mama wanaougua Fisgtula.
“Sisi
tunaamini, miongoni mwa watoto watakaotibiwa, miongoni mwa akina mama
watakaotibiwa wako wanachama wetu ambao kupitia mbio hizi tunakwenda kuwagusa.”
Amefafanua Bw. Mwakifulefule na kjuongeza….Sisi peke yetu tungehitaji fedha
nyingi kufanikisha suala hili, lakini tunapoungana pamoja, sisi PSSSF, CRDB na
wadau wengine wanaounga mkono mbio hizi basi changamoto za watoto na akina mama
hawa zinakwenda kutatuliwa.” Amesisitiza.
Akitoa
neno la shukrani, mwakilishi kutoka CRDB Bank Bi. Joycelean Makule, ameishukuru PSSSF kwa msaada huo ambao amesema
unakwenda kusaidia mipango muhimu ya afya ili kusaidia jamii ya Watanzania.
“Mbio
hizi zimeanzishwa ili kuhakikisha watanzania wenyewe tunajenga utamaduni wa
kuweza kutatua matatizo yanayotuzunguka, na hili tumeona ni jukwaa zuri
kushirikiana na watanzania, na mwaka huu tumeweza kushirikiana na jumla ya watu
8000.” Amesema.
Aidha,
amesema mbio za CRDB Marathon zinatarajiwa kufanyika Agosti 18, 2024, jijini
Dar Es Salaam.
Meneja
Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa
Umma (PSSSF), Bw. Yesaya Mwakifulefule (kulia), akimkabidhi mfano wa Hundi
yenye thamani ya shilingi milioni 10, Mwakilishi wa CRDB Bank Foundation, Bi.
Joycelean Makule, kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye maradhi ya
moyo na akina mama wanaosumbuliwa na changamoto ya Fistula, kupitia mbio za CRDB
marathon. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar Es Salaam Agosti 16, 2024.