Kiongozi wa Wanawake Kijana Hellen Sizya wakati wakizungumza na waandishi wa wahabari jijini Dar es salaam wakitoa tamko la wanawake vijana viongozi kupinga mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Ngono kifungu cha 10(b)
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Msichana Initiative Sara Beba wakizungumza na waandishi wa wahabari jijini Dar es salaam wakitoa tamko la wanawake vijana viongozi kupinga mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Ngono kifungu cha 10(b).
…………………..
NA MUSSA KHALID
Wanawake vijana Viongozi kwa ushirikiano na Mtandao wa Kupinga Rushwa ya Ngono nchini wamemuomba Rais wa Tanzania Samia Suluh Hassan kutopitisha mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa hiyo kifungu cha 10 (b) endapo Bunge litapitisha.
Pia wamesema hawatonyama kutokana na suala la rushwa linawathiri katika maeneo mbalimbali kuanzia majumbani,vyuoni,makazini,kwenye sanaa,michezo na kwenye vyama vya siasa.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Kiongozi wa Wanawake Kijana Hellen Sizya wakati wakizungumza na waandishi wa wahabari ambapo amesema kuwa wameshangazwa na kuendelea kupuuzwa kwa mapendekezo ya kufutwa kifungu cha nyongeza cha 25(b) kilichompoka mhanga.
Aidha amesema kuwa kwa kuzingatia tafiti zilizofanywa na TAKUKURU kwa kushirikiana na wanamtandao wanaopinga rushwa ya Ngono hivyo kama wanawake vijana wanatambua ukubwa wa tatizo hilo.
‘Tunatambua kuwa Sheria ya kupambana na Rushwa ya Ngono intoa tafsiri sahihi inayotofautisha Rushwa ya Ngono na Rushwa Nyingine ya kwamba Rushwa ya Ngono inahusisha wenye Mamlaka kutumia vibaya Mamlaka yao kudai Ngono kama sharti la kumpa mhanga haki stahiki zake na kumpendelea mhanga kumuahidi kumtunuku’amesema Sizya
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Msichana Initiative Sara Beba amewashauri wabunge kutambua kuwa vijana ni wengi zaidi na ndio wanaathirika kwa kiasi kikubwa hivyo ni vyema waacha kupitisha kifungu hicho kwa sababu kinawakandamiza.
‘Bunge letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo linatuwakilisha sisi,lisipitishe mabadiliko,kwani kazi ya Bunge ni kutunga sheria za kulinda Haki na sio kutunga sheria ya kumlinda Mhalifu’amesema Sara
Pia ametoa wito kwa Watanzania,watetezi wa haki za bianadamu hususani za wanawake na watoto wa kike kupinga vikali kuingizwa kwa kifungu cha 10(b) kwenye mswada huo