Hospital ya Rufaa ya kumbukumbu ya Mwalimu J.K. Nyerere Mkoani Mara, inatarajia kuanza kutoa huduma ya upasuaji wa Mgongo wazi pamoja na vichwa vikubwa kwa watoto baada ya kukamilika kwa mafunzo yanayotolewa na madaktari bingwa kutoka hospital ya kanda ya Bungando.
Akizungumza kuhusu huduma hiyo Daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mgongo kutoka hospital ya kanda ya Bungando Dk. Gerald Mayaya amesema wameanza kutoa huduma hiyo inayoendana na mafunzo ili kusaidia wananchi Kupata huduma karibu badala kusafiri umbali mrefu.
“Lengo kubwa ni kuisaidia madaktari waweze kutoa huduma kwa watoto wanaokuja huko mfano kama Bungando tunaona watoto 700 kwa mwaka lakini kati ya hao watoto 50 wanatokea Mkoa wa mara kwa hiyo wakiwa na uwezo wa kuwahudumia itasaidia kupunguza rasilimali Muda na fedha”Alisema Dk. Gelard Mayaya.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Mwanangu Development Tanzania Walter Miya amesema lengo la kutoa mafunzo hayo kwa hospitalI za rufaa za mikoa ni kuhakikisha wanawajengea Uwezo madaktari watoa huduma kwa wananchi wa mkoa wa Mara na maeneo mengine huku baadhi ya wananchi walionufaika na huduma hiyo wakipongeza kwani imesaidia kuboresha na kutoa unafuu wa maisha kwa watoto wao