Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Emmanuela Kaganda akizungumza katika baraza hilo
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Jeremiah Kishili akizungumza katika.baraza hilo
Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Mwalimu Zainabu Makwinya akizungumza katika baraza hilo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Meru Mwalimu Zainabu Makwinya akizungumza katika baraza hilo.
……
Happy Lazaro ,Arusha .
.Mkuu wa wilaya ya Arumeru ,Emmanuela Kaganda amewataka madiwani wa halmashauri ya meru kuendelea kuimarisha na kusimamia ukusanyaji wa mapato vilivyopo katika maeneo yao ili kuendelea kuipatia halmashauri hiyo mapato zaidi.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na madiwani katika baraza la kufunga mwaka wa fedha 2023/24.
Aidha amewataka pia kuendelea kuangalia vyanzo vya mapato vilivyopo na uvunjifu wa mapato kwenye miradi hiyo ikiwemo kwenye maeneo ya ujenzi, madini na hata kwenye minada na kuhakikisha kila mahali fedha zinakusanywa upasavyo na zinapelekwa sehemu sahihi na kwa wakati .
Hata hivyo Kaganda amempongeza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo pamoja na madiwani hao kwa namna ambavyo wanafanya kazi nzuri katika kuhakikisha mapato ya halmashauri yanaendelea kuongezeka kila wakati kutokana na vyanzo mbalimbali vilivyopo.
“Nawaomba sana waheshimiwa madiwani mhakikishe kuwa maeneo yenu yanakuwa safi kila wakati ,na mkumbuke kuwa uchaguzi wa serikali.za mitaa umekaribia hivyo mtumie.nafasi zenu ipasavyo kuhakikisha mnahamasisha wananchi wenu katika.kushiriki uchaguzi huo ipasavyo.”amesema Kaganda.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Jeremiah Kishili amesema kuwa,swala la.kusimamia mapato katika halmshauri hiyo watalisimamia kwa kushirikiana na madiwani wote ili kuhakikisha mapato yanaongezeka katika halmashauri hiyo.
Aidha amewataka madiwani mbalimbali waliochaguliwa katika kamati zao kushirikiana kwa pamoja katika kujadili maswala mbalimbali ya maendeleo na kuhakikisha wanakuwa na majibu ya maswali watakayoulizwa kwenye baraza.
Nao baadhi ya madiwani waliochaguliwa katika kamati mbalimbali,akiwemo diwani wa kata ya kikatiti Kisali Nyiti na diwani wa kata ya Leguruki Nathan Sikawa wamesema kuwa wamesema kuwa watafanya kazi kadri watakavyoweza huku wakiwaomba madiwani kuwapa ushirikiano katika kusimamia fedha za halmashauri.
Sambamba na hilo baraza hilo limefanya mkutano wa kawaida wa mwaka wa halmashauri lililoenda sambamba na kuteua wajumbe wa kamati za kudumu za halmashauri kwa mwaka 2024/2025 na kujadili taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa halmashauri ya wilaya hiyo kwa mwaka uliopita 2023/2024.