Na Neema Mtuka
Rukwa
Baadhi ya wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na dira ya taifa ya maendeleo ya 2050 ambapo wameitaka serikali kuongeza juhudi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo kuboresha miundombinu ya barabara ,maji ,umeme madarasa pamoja na na hospitali.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa akiwemo Didas Mbalawa amesema serikali ihakikishe amani na utulivu vinakuwepo kwa kushirikisha vyama vya siasa katika kujadili maendeleo pamoja na kudumisha ushirikiano kati ya sekta binafsi na taasisi za serikali.
Huku Mwl Kaitani Milanzi amehimiza ushirikiano kwa serikali katika hatua mbalimbali zinazoendelea za kuleta maendeleo kwa wananchi pamoja na maboresho kupitia miradi ya maendeleo na kuhakikisha wanawatumia wataalamu katika sekta zote.
Wajumbe wa kamati ya ushauri ya wilaya ya Nkasi wakiongozwa na Mwenyekiti wa kikao Levocatus Chikala aliyemwakilisha mkuu wa wilaya Peter Lijualikali amesema wao wamefanya tathimini ya maendeleo ya dira ya taifa kwa kuangazia Nyanja za kiuchumi ,kisiasa ,utawala bora pamoja na amani na utulivu .
Amesema kuwa lengo la tathimini hiyo ni kuwa shirikisha wananchi kutoa maoni yao juu ya dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2050 na kutoa mapendekezo yao kulingana na dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 na ile ijayo ya mwaka 2050.
“Kila mwananchi anayo haki ya kutoa maoni na mapendekezo yake ndio maana tumewashirikisha wananchi kutoka makundi mbalimbali wakiwemo walemavu ,vijana ,mashirika na asasi za kiraia lengo ni kutaka kuwakutanisha pamoja na kuangalia mustakabali wa dira ya taifa ya maendeleo ijayo”.Amesema Chikala.
Kupitia kikao hicho wajumbe wameipongeza serikali kwa utekelezaji mzuri wa dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 ambapo serikali imeleta maendeleo makubwa kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara ,maji na umeme.
Aidha wajumbe hao wamesema serikali imehakikisha amani na utulivu kwa kushirikisha makundi mbalimbali yakiwemo Taasisi za kidini sekta binafsi bna taasisi za kiserikali.
Pamoja na hayo wajumbe wametoa mapendekezo ya dira ya raifa ya maendeleo kwa mwaka 2050 iendelee kujikita katika vipaumbele stahiki ikiwa ni pamoja na kubnoresha sekta ya usafiri wa anga na maji ,sekta ya kilimo na kuwa na mpango kazi wenye vipaumbele kulingana na mazingira .
Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Steward Vidoga amewashukuru wajumbe kwa kutoa maoni yao na mapendekezo ya dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2050 na kuwataka kuendelea kulinda amani na utulivu sambamba na kusimamia maadili kwa kuzingatia usawa bila kujali itikadi zozote dini wala ukabila.