Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeshiriki Kikao cha kuwasilishwa kwa Miswada ya Sheria.
Miswada iliyowasilishwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ni pomoja na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Shule ya Sheria Tanzania, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ya mwaka 2024, na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Na 2 wa mwaka 2024.
Kikao hicho cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kimefanyika tarehe 14 Agosti 2024 Bungeni Jijini Dodoma.