Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo (Mb) ametembelea Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Masharki (EAC) Mhe. Veronica Nduva Ofisini kwake jijini Arusha.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Londo alimuhakikishia Mhe. Nduva ushirikiano na kumuelezea kuwa Tanzania itashiriki katika masuala yote yanayohusu Jumuiya ya EAC kwa uzito unaostahiki.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kujitambulisha na kufahamiana baada ya Mhe. Londo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika mwezi Julai 2024.
Mhe. Londo aliongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Stephen Mbundi.