Ashrack Miraji Same (Full shagwe media) Kilimanjaro
Zaiadi ya Shilingi Bilioni nane (8) kutumika kufanya ukarabati wa kituo cha kupoozea Umeme cha Same kuondoa mfumo wa zamani na kuweka mpya wa kisasa ambao utasaidia kuongeza ufanisi na kufanya Wilaya hiyo kuwa na Umeme wa uhakika zaidi, mradi ambao unatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa ufadhiri wa Bank ya Maendeleo ya Ufaransa (ADF).
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi huo Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amesma kukamilika kwa mradi huo pamoja na kuongeza Umeme kwenye Wilaya lakini pia unatoa fursa kwa wawekezaji hasa Viwanda kuja kuwekeza Same kwani bado kunauhitaji mkubwa wa wawekezaji hasa wa Viwanda.
Aidha Mradi huo utaongeza Umeme mwingi katika Wilaya ya Same kwani wa sasa uliopo ni MVA 5 ambao unazalishwa na Transfoma moja pekee lakini mradi huo unatarajia kuongeza Transfoma mbili (2) zenye ukubwa wa MVA 10 kwa kila moja sawa na ongezeko la MVA 20 na kufanya kituo hicho kuwa na Transfoma tatu (3) ambazo zinazalisha Umeme wa MVA 25.
“Sisi wakazi wa Same kwa dhati ya Mioyo yetu tunakushukuru sana sana Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo unaendelea kutupatia fedha za miradi mbalimbali, kwetu sisi kuwa na huduma ya Umeme ya uhakika ni nyenzo mojawapo ya kukua kwa uchumi wa Wilaya yetu na Mwananchi mmoja mmoja”, Alisema DC Kasilda.
Pia amemuelekeza Mkandarasi kuhakikisha maradi unatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa kwenye ujenzi wa miradi ya Serikali lakini pia ukamilike kwa wakati kwa mujibu wa mkataba ili wakazi wa Same wanufaike na Uwekezaji huu mkubwa.