Mkurugenzi Mkazi wa Bia ya Heineken Tanzania, Obabiyi Fagade akiwa na Meneja wa Masoko wa kampuni ya Bia ya Heineken Tanzania, Lilian Paschal wakati wa muendelezo wa burudani ya “Afterwork by Heineken” ikiwa ni sehemu ya kuwaweka pamoja wadau wa bia hiyo ili kupata burudani na kubadilishana mawazo.
………………..
Kampuni ya bia ya Heineken Tanzania inaendelea na burudani yake ya “Afterwork by Heineken” hii ni burudani kwa wadau wake baada ya kazi na kuweza kupumzika pamoja kwa kupata kiywaji chao cha Heineken na burudani ya muziki.
Hili ni tukio linalojumuisha watu pamoja baada ya siku ndefu ya kazi. Tukio hili lenye msisimko limeanzishwa ili kukuza mtindo wa maisha unaoleta uwiano mzuri kati ya kazi na mapumziko, kwa kutoa nafasi ya kuburudika na kushirikiana na wengine. Ahadi ya Heineken kwa watumiaji wake nchini Tanzania ni kuonekana wazi kwani chapa hii inaendelea kutoa uzoefu bora kwa kuthibitisha nafasi yake kama mtetezi wa usawa wa maisha na kazi.
Kama unatafuta kupumzika au kujenga mtandao na watu wenye mawazo yanayofanana, Afterwork by Heineken ni sehemu sahihi ya kubadilishana mawazo.
Tukio hili lilifanyika ukumbi wa Boardroom Sinza wiki iliyopita ikiwa ni tukio lake la pili tokea kuanzishwa kwake, Tukio la kwanza lilifanyika Samaki Samaki.