WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe Deogratius Ndejembi amefanya kikao kazi na wataalamu wa Idara ya Maendeleo ya Makazi pamoja na Idara ya Upimaji na Ramani Agosti 13, 2024 ambacho kimefanyika Makao Makuu ya Wizara Mtumba jijini Dodoma.
Katika kikao hicho Mhe. Ndejembi amewataka wataalamu wa idara hizo kufanya kazi kwa weledi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo ya taaluma zao hatua inayowasaidia kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya wizara ili kuwahudumia Watanzania.