WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amepiga marufuku vitendo vya udhalilishaji dhini ya walimu napiga marufuku na kusisitiza kuwa kuanzia sasa nataka aone walimu wakiwa na furaha.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kukabidhi magari kwa makatibu wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu yaliyokabidhwa katika mji wa Serikali Mtumba.
Alisema Rais Samia Suluhu Hassan hataki kusikia walimu wanapata changamoto yoyote.
“Mimi mwenyewe kama Waziri mwenye dhamana kwenye sekta hii nataka nione walimu wanafuraha wakati wote, nataka nione walimu wakifurahia serikali yao wakati wote.
“Katika kipindi changu hiki sitegemei kuona mwalimu akinyanyaswa mwalimu akionewa kwasababu ambazo mtendaji katika eneo hilo anafanya yenye mwenyewe makusudi.”
Mchengerwa aliongeza: “nawataka wakurugenzi wasaidizi, makatibu wasaidizi wa Tume ninao wakabidhi magari leo nendenei mkafuatilie yanayoendelea kwenye maeneo yenu.”
“Kama kuna vitendo vya udhalilishaji dhini ya walimu napiga marufuku kuanzia sasa nataka tuone walimu wakiwa na furaha.”
“Huu ni ujumbe wangu kwa walimu kote nchi serikali inayoongozwa na Rais Samia anatamani kuona kila mtumishi ndani ya TAMISEMI anafurahi na kutabasamu, nendeni mkatibu kero za walimu, nendeni mkamalize changamoto za walimu.”
Aidha, Mchengerwa ameielekeza Tume kuwa karibu na walimu na kuwasikiliza na kutatua kero zao.
“Tume kazi yake ni kukaa na walimu na katika kipindi changu sitegemei kusikia mwalimu anamsongo wa mawazo hamjamfikia, msisubiri mimi nipigiwe simu.”
Aliseka kwa sasa Tume haina visingizio kwani imeshapata bodi na kusisitiza kuwa hataki kusikia mtumishi TAMISEMI ana hofu na serikali yake.
“Wenye zile kero ngumu ngumu wasaidie, sijui uhamisho kwa aliyekidhi vigezi shughulikieni, waliofukuwa washaurini taratibu za kufuata na msijiweke mbali na watumishi.”
Alisema kwa sasa amekuwa akipokea kero nyingi za walimu na kuitaka Tume kujitahidi kuzifanyia kazi kero za walimu kwa haraka.
Mchengerwa pia amesisitiza uwajibikaji na kutambuwa majukumu ya kiutendaji kwa watendaji katika maeneo yao ya kazi kwani ndio msingi wa utendajikazi.