Tanzania imehitimisha mashindano ya Olimpiki ya Paris 2024 bila kuambulia kitu baada ya wakimbiaji wake Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri kushindwa katika mbio za Marathon kwa Wanawake ambazo zimehitimisha rasmi michezo hiyo leo.
Kundi kubwa la waTanzania waishio Ufaransa, wakiongozwa na mshangiliaji mashuhuri Bongo
Zozo, lililipuka kwa nderemo wakati Shauri akiingia uwanjani akiwa katika nafasi ya 40, akitumia saa 2:31:58.
Kwenye mbio za kuhitimu kushiriki Olimpiki Shauri alikimbia muda wa saa 2:18:41
Sakilu alijitoa katika kilomita 18, baada ya kuzidiwa na maumivu aliyoyapata baada ya kukanyagwa mguu wake wa kushoto na mkimbiaji A. Beriso Shankule wa Ethiopia kilomita nne tu baada ya kuanza mbio.
Ndiyo kusema Sakilu, ambaye kwenye mbio za kuhitimu kushiriki mashindano ya Olimpiki alitumia muda wa saa 2:21:27, alikimbia na maumivu kwa kilomita 14 kabla ya kuzidiwa.
Mshindi wa mbio hizo alikuwa Sifan Hassan ambaye alipigana vipepsi na Tigst Assefa zikiwa zimesalia mita 150 katika mbio za marathon za wanawake, kisha akampita na kushinda mbio za medali yake ya tatu ya masafa marefu ya Olimpiki.
Hassan, mwanariadha mzaliwa wa Ethiopia anayekimbilia Uholanzi, alimaliza katika muda wa rekodi ya Olimpiki ya saa 2, dakika 22, sekunde 55. Assefa alishinda medali ya fedha kwa Ethiopia, sekunde tatu nyuma, na Mkenya Hellen Obiri alinyakua shaba.
Timu ya Ethiopia ilifanya maandamano kutaka Hassan afutwe kwa kuzuiwa, lakini yalikataliwa na Mahakama ya Rufaa. Ilionekana kana kwamba Assefa alikuwa akimzuia Hassan, ambaye alizuiliwa mara mbili kabla ya kulishana vipepsi.