Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe 10 hadi 11 Agosti, 2024 Mkoani Mkoani Mwanza.

Washiriki
wa Mafunzo yaliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura mkoani Mwanza, wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa
chama cha siasa na kutunza siri wakati wa kutekeleza majukumu yao. Mafunzo hayo
yameanza leo tarehe 10 Agosti, 2024 na yamehusisha Mratibu wa Mkoa wa
Uboreshaji wa Daftari, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Uchaguzi, Maafisa TEHAMA
na Maafisa Ugavi wa halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga. Uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Mwanza na Shinyanga utafanyika kuanzia
tarehe 21 hadi 27, Agosti, 2024 ambapo
vituo vitafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Asina Omari akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo.
Mmoja wa wakufunzi kutoka Idara ya TEHAMA na DAFTARI akitoa somo la ujazaji wa fomu mbalimbali zinazotumika wakati wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mmoja wa wakufunzi kutoka Idara ya TEHAMA na DAFTARI akitoa somo la ujazaji wa fomu mbalimbali zinazotumika wakati wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetaka
watendaji wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mkoani Mwanza
na Shinyanga kuhakikisha wanatunza vifaa vya uandikishaji ili vikaweze kutumika
maeneo mengine nchini.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele wakati akifungua mafunzo
ya siku mbili kwa Waratibu wa Uandikishaji wa mkoa, Maafisa Waandikishaji,
Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi
na Maafisa TEHAMA wa halmashauri yaliyoanza leo tarehe 10 hadi 11 Agosti, 2024 Mkoani
Mkoani Mwanza.
Mafunzo kama hayo pia yamefunguliwa Mkoani Shinyanga
na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufaa(Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk leo
mkoani humo.
“Kwa kusisitiza, ni muhimu kutekeleza
majukumu yenu kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya
uandikishaji hasa ikizingatiwa kuwa, vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa
sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini,”
alisema Jaji Mwambegele.
Amesema kutokuwa makini katika utunzaji wa
vifaa hivi kutapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hili muhimu na
amewataka kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili muweze
kuyafanyia kazi wakati zoezi litakapokuwa limeanza.
Aidha, Jaji Mwambegele amesema matokeo bora
ya zoezi hili yanategemea uwepo wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa
uboreshaji, serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi.
“Ninawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa
karibu na Tume wakati wote mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu na ikiwa
mnahitaji ufafanuzi au maelekezo yeyote, msisite kuwasiliana na Tume,” alisema
Jaji Mwambegele
Mapema kabla ya kuanza mafunzo hayo,
washiriki walikua kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri mbele ya
Hakimu Mkazi wa Mwandamizi wa Wilaya Ilemela, Christian Mwalimu.
Mafunzo hayo yanahusisha namna ya ujazaji wa
fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voters Registration
System – VRS) ili waweze kupata uelewa wa pamoja utakaowapa fursa ya kutumia
kwa ufasaha mfumo huo pamoja na vifaa vingine vya kuandikisha wapiga kura.
“Mafunzo haya, yanawajengea umahiri wa
kuwafundisha Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata kisha nao watatoa
mafunzo hayo kwa Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki na Waandishi Wasaidizi
ambao ndio watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni,” alisema Jaji Mwambegele.
Aidha, Maafisa TEHAMA watapatiwa mafunzo
maalum ya jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiufundi
(Troubleshooting) endapo zitajitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji wa wapiga
kura vituoni.
Katika hatua nyingine, Jaji Mwambegele
amewaambia watendaji hao kuwa wakati wa
uboreshaji wa Daftari mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika
vituo vya kuandikisha wapiga kura jambo ambalo litasaidia kuleta uwazi katika
zoezi zima lakini pia mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika
hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima.
Jaji Mwambegele alitoa angalizo kwa mawakala
hao kutoka vyama vya siasa kuwa
hawaruhusiwi kuwaingilia watendaji wakati wote wa utekelezaji wa
majukumu yao vituoni.
Tume tayari imeanza zoezi la uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo mzunguko wa kwanza ulianza kwa mikoa ya
Kigoma, Katavi na Tabora kuanzia Julai 20 hadi 26,2024 na mzunguko wa pili
unaendelea katika mikoa ya Kagera na Geita ambao ulianza Agosti 5 hadi 11 mwaka
huu, na kauli mbiu ya uboreshaji ni
“Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura Ni Msingi Wa Uchaguzi Bora.