Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Joseph Kilangi, ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo – Nane Nane yanayoendelea visiwani Zanzibar katika viwanja vya Kizimbani-Dole, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kilangi alipata fursa ya kujifunza kuhusu majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na Benki Kuu ya Tanzania.
Maonesho hayo ya saba (7) tangu kuanza kufanyika visiwani Zanzibar, yanabebwa na kauli mbiu “Kilimo ni utajiri, kila mtu atalima,” na yanaendelea kufanyika hadi tarehe 14 Agosti, 2024.