Tarehe 08 Agosti 2024, Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji alikutana na Mhe. Manuel José Gonçalves , Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jamhuri ya Msumbiji kwenye Ofisi za Wizara hiyo ilizopo Jijini Maputo.
Wakati wa mazungumzo hayo, Viongozi hao walizungumza masuala mbalimbali ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji.
Aidha, kupitia mkutano huo, Mhe. Balozi Kasike alikumbushia ombi la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuungwa mkono na Serikali ya Jamhuri ya Msumbiji wakati wa Uchaguzi wa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika ambapo Tanzania imemsimamisha Mhe. Dkt Faustine Ndungulile (Mb). Uchaguzi wa Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika utafanyika Jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo tarehe 27 Agosti, 2024.
Imetolewa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Maputo.
09 Agosti, 2024