Serikali mkoani Njombe imesema inakabiliwa na upungufu wa watumishi 4,747 kati 7350 waliyopaswa kuwepo kazini katika hospitali 16 ,vituo vya afya 42 pamoja na zahanati 260 za mkoa huo jambo ambao limekuwa na athari kwenye utoaji wa huduma na kisha kuweka wazi uhaba wa wataalamu wa mionzi na kinywa na meno.
Katika mahafali ya 9 ya chuo cha afya mgao Mganga mkuu wa mkoa wa Njombe Dr Juma Mfanga amesema hadi sasa Njombe inawatumishi 2603 kati ya elfu 7350 katika vituo 361 vya kutoa huduma za afya huku upungufu mkubwa ukiwa kwenye wataalamu wa mionzi na kinya na meno na kisha kuwataka wazazi na wanafunzi kuitazama fursa zilizopo katika maeneo hayo katika kipindi hiki ambacho serikali inaendelea kutangaza ajira.
Wakati idadi ya wasomi wasio ikizido kuongezeka na serikali kuendelea kuajiri ili kupunguza ombwe la watumishi katika kada ya afya,Ofisa Utumishi Chuo cha afya Mgau Deus Kuba na Mkurugenzi wake Dr Adelitis Mgao wanasema ajira zitakuwa changamoto katika kada hiyo pindi tu watu wakapo goma kufa na magonjwa kuacha kuibuka ulimwenguni hivyo wanafunzi wasiofu kuhusu ajira.
Kwa upande wao baadhi ya wahitimu akiwemo Sara Mtenzi na Geofrey Kaunda wanasema wajiandaa vyema kwenda kukabiliana na changamoto ya ajira kwa kufungua maduka ya dawa na kujitolea ili kuhudumia watanzania. Takribani wahitimu 314 wamehitimu na kupatiwa vyeti vya taaluma tayari kwa huduma katika jamii.