Na Prisca Libaga Arusha
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kinga kwa wananchi waliohudhuria Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kikanda viwanja vya Themi vilivyopo Njiro mkoani Arusha.
Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ni “_Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi_” . Mgeni rasmi wa kilele cha maadhimisho hayo kikanda alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga.
Aidha, DCEA Kanda ya Kaskazini imewaasa wakazi wa mikoa ya kanda ya Kaskazini kuachana na matumizi pamoja na kilimo haramu cha dawa za kulevya hususani kilimo cha bangi na mirungi. Pia, imewahamasisha wananchi kushirikiana na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya nchini kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga namba ya simu ya bure 119.