Sekretarieti ya maadili imewashauri wakulima, wafugaji kuwa waadilifu katika utendaji wa shughuli zao ili waweze kufanikiwa.
Ushauri huo umetolewa Leo Ijumatano Agosti 7, 2024 na Kamishina wa Sekretarieti hiyo Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi wakati akizungumza mara baada ya kutembelea banda la Sekretarieti ya maadili katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea kufanyika Nzuguni Jijini Dodoma.
Amesema wamekuja kushiriki kwenye maonesho hayo ili kujitambulisha na kuujukisha umma kuhusiana na majukumu wanayoyafanya.
“Maadili ni kitu kinachowahusu watu wote ikiwemo wakulima hivyo ili mtu aweze kufanikiwa katika shughuli mbalimbali anazozifanya lazima awe na maadili kwani bila uadilifu hakuna vitu haviwezi kuendelea”, amesema Mwangesi
Ameeleza kuwa viongozi wanahusika na watu na wananchi pia wanatakiwa kuyajua majukumu ya viongozi ili watakapo vunja majukumu yao wawape taarifa.
Gracness ni mwanafunzi wa shule ya msingi Mkonze Jijini Dodoma amesema amekuwa mwanachama wa klabu ya maadili kwa muda wa miezi mitatu na amefanikiwa kujiamini pamoja na kupata watu wengine wakuwaeleza masuala ya kimaadili