Wadau wa elimu,Wanafunzi na wakufunzi wa vyuo wameiomba serikali kutanua wigo mikopo ya elimu inayotolewa na serikali kwa wanafunzi wa vyuo vya kati badala ya kujikita kwenye kozi chache za kipaumbele ili kunusuru ndoto za watoto masikini zinazoishia njiani kwasababu ya kukosa fedha ya kujikimu na steshenari pamoja na watoto wakike ambao wanajikuta wakitumbukia kwenye biashara ya ngono ili kupata fedha.
Wakiweka bayana athari zinazowakuta wanafunzi wa vyuo vya kati wanaotoka familia duni wadau akiwemo Buteye Dotto ambae ni Mkuu wa chuo cha Luheti katika mahafali ya 24 ya Chuo hicho wamesema wanafunzi wengi wanajikuta wakitumbukia kwenye biashara ya Ngono na wengine kUshindwa kuendelea na masomo kwasababu ya kushindwa kumudu Mahitaji chuoni hivyo wanaomba serikali kutanua wigo wa kozi zinazonufaika na mikopo ili kuokoa mamia ya ndoto zinazokufa kwa kushindwa kuendelea na masomo.
“Tumekuwa tukisaidia wanafunzi wasio jiweza na wengine hushindwa kumaliza masomo kwasababu ya kukosa fedha ya ada na kujikimu hivyo wanamuomba Rais Samia kutanua wigo wa fursa hiyo ya mikopo ambayo ameanza kutoa kwa mara ya kwanza”alisema Buteye Doto.
Kwa upande wao wanafunzi akiwemo Brenda Shayo amesema wanafunzi wa Vyuo vya kati wanapata elimu katika mazingira magumu kwasababu wapo wanaotoka katika mazingira magumu na kisha kuomba serikali kuanza kutoa mikopo kwa kozi zote badala ya kuangalia kozi za vipaumbele ili kuepusha watoto wa kike kujiingiza kwenye biashara ya ngono ili waweze kujikumu na wakiume kutumbukia kwenye makundi hatarishi.
Wakati wadau wakitoa mapendekezo yao ili kuboresha sekta ya elimu hususani kwa vyuo vya kati ,Mwakilishi wa mkuu wa Mkoa Nae Juma Sweda ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Makete anasema kwakuwa bado serikali inaendelea na ujenzi wa vituo vya afya,zahanati na hospitali hata suala la ajira zitaendelea kutolewa na kisha kutoa rai kwa wahitimu kutosita kujitolea kipindi ambacho watakuwa wakisubiri ajira za serikali.
Katika hatua nyingine Sweda amehimiza wahitimu kuanza kufikiria zaidi shughuli za ujasiriamali ili kukabiliana na tatizo la ajira ambalo linakuwa kila kukicha kutokana na ongezeko la wasomi nchini na kisha kuwataka kuunda vikundi ili wapewe mikopo ya wajasiriamali ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri.
Awali mhashamu askofu wa jimbo katoriki Njombe Eusebio Kyando na Mkurugenzi wa chuo cha afya LUHETI-Padre Alexanda Mlewa wamewakumbusha wahitimu wa kada afya kutekeleza majukumu yao pindi wawapo kazini huku pia wakiomba serikali kutazama kwa jicho tatu tatizo la ajira.