Na Mwandishi wetu.
Makamo Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM-Taifa)Rehema Sombi amekabidhi Vyerehani viwili kwa Chuo Cha Ufundi stadi Veta,Furahika ili kuboresha mazingira ya ufundishaji kwa vitendo chuoni hapo.
Akikabidhi vyerehani hivyo Jijini Dar Es Salaam Kwa niaba ya Sombi,Mwenyekiti wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Ilala Juma Misungu amesema kukabidhiwa kwa msaada huo ni utekelezaji wa ahadi aliyoahidi Bi Sombi katika mahafali ya 18 ya Chuo hicho mwezi April mwaka huu.
“Leo tumetimiza lengo la kuona namna ya kuwasaidia vijana hasa wanaosoma fani ya ushonaji ambapo kwenye mahafali yaliyofanyika hapa chuoni Aprili 27 mwaka huu,Makamo mwenyekiti wetu wa umoja wa Vijana Taifa aliahidi kutoa cherehani mbili na akanikabidhi hela keshi pale pale na tukaagiza vifaa hivi na leo vimefika tumevikabidhi kwa Mkuu wa Chuo ni faraja kwetu Kama vijana kusaidia vijana wenzetu kupata nyenzo za kujisomea”amesema Bw Misungu
Ameutaka uongozi wa Chuo hicho kuvitunza vifaa hivyo vya ushonaji ili kusaidia katika kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wanafunzi wengine wanaopata mafunzo ya ushonaji katika Chuo Cha Furahika.
Aidha amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendeleza uhusiano wake na Chuo hicho ambacho hutoa mafunzo bila malipo ili kuhakikisha vijana wanapata mafunzo kwa vitendo na hatimaye kujiajiri ama kuajiriwa na kukuza uchumi wa Taifa.
Akizungumza Mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo (Vyerehani)Mkuu wa Chuo Cha Cha Ufundi stadi Furahika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Chuo hicho Dkt David Msuya ameushukuru uongozi wa UVCCM-Taifa kupitia Makamo mwenyekiti Wake Rehema Sombi kwa kutimiza ahadi yake ya kutoa msaada huo na kuongeza Kuwa vitaboresha utoaji wa mafunzo ya ushonaji kwa vitendo chuoni hapo.
“Nimesikia Furaha Sana Leo kukabidhiwa vifaa hivi na ukizingatia darasa la Ufundi hapa chuoni kwetu Lina wanafunzi zaidi ya 100 hivyo Vyerehani hivi vitatusaidia katika masomo,na niipongeze serikali ya CCM kupitia Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kuwa na viongozi waaminifu wanaotimiza ahadi zao”amesema
Dkt Msuya amewaomba wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuwasaidia vifaa mbalimbali ikiwemo kompyuta na vyerehani zaidi kwani hatua ya chuo hicho kutoa elimu bila malipo ni kuamini Kuwa kufeli darasa la saba au kidato Cha nne siyo mwisho wa maisha kwani elimu ya Ufundi ina msaada mkubwa kwa vijana na kuwaepusha kihalifu ikiwa ni pamoja na matumizi ya dawa za kulevya na kuuza miili.
Aidha ameongeza Kuwa Chuo hicho kimeanzisha program maalum ya masomo ya jioni kwa watu wazima hasa akina mama katika fani za ushonaji,upishi wa keki na Upambaji hivyo amewasihi wazazi kuwapeleka watoto hao kupata mafunzo ya Ufundi katika Chuo hicho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mivinjeni uliopo kata ya Buguruni Manispaa ya Ilala Jijini Dar Es Salaam ambapo ndipo kilipo Chuo Cha Ufundi stadi Veta Furahika Bw Fadiga Legele amesema wao Kama viongozi wanafarijika kwa uwepo wa Chuo hicho katika Mtaa wao na wataendelea kutoa ushirikiano Kama serikali ya Mtaa na Kuwa mabalozi wa Chuo hicho.