NA JOHN BUKUKU, DODOMA
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetenga fedha kwa ajili ya Taasisi za fedha ikiwemo mabenki ili waweze kuwakopesha wananchi wanaofanya shughuli za kilimo kwa riba nafuu.
Akizungumza leo August 5, 2024 katika Maonesho ya kimataifa ya kilimo Nanenane yanayofanyika Nzuguni jijini Dodoma, Afisa Mkuu Mwandamizi Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Deogratius Mnyamani, amesema kuwa lengo ni kuhakikisha wakulima wanapata mikopo kwa gharama nafuu
Amesema kuwa ili mkulima apige hatua katika mafanikio anatakiwa kuwa mipango pamoja na kufanya uwekezaji katika sekta ya kilimo jambo ambalo litaleta tija na kufikia malengo husika.
Amesema kuwa lengo ni kuhakikisha wakulima waweze kukopeshwa kwa riba nafuu katika taasisi za fedha pamoja na mabenki katika utekelezaji wa shughuli zao.
“Pia kuna fursa mbalimbali kwa wale ambao wanataka kuanzisha biashara za huduma za fedha katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini kwa kuwakopesha wakulima wadogo”
Hata hivyo ametoa wito kwa taasisi za fedha kutoa mikopo kwa wakulima kwa kuzingatia riba nafuu ili kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa.