Kaimu Mkurugenzi wa Tawi la BoT Zanzibar, Bw. Abdullah Mansour akimkaribishe Rais Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi katika banda la maonesho la BoT katika viwanja vya Kizimbani.
………………..
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, siku ya Jumamosi tarehe 03 Agosti, 2024 alifungua rasmi maonesho ya Saba ya Wakulima (Nane nane) katika viwanja vya Kizimbani Dole, Mkoa wa Mjini Magharibi, Visiwani Zanzibar.
Katika sherehe hizo Mhe Rais alisisitiza dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanizbar katika kuleta mageuzi ya kweli ya kilimo, kwa kukifanya kuwa chenye tija.
“Serikali ninayoingoza imedhamiria kufanya mageuzi makubwa ya kilimo hapa nchini, kilimo chetu sasa kitakuwa chenye tija kutoka shambani hadi kumfikia mlaji”, alisema Rais Dk Hussein Mwinyi.
Pia Rais Dkt. Mwinyi alitembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania, ambapo alikaribishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Tawi la BoT Zanzibar, Bw. Abdullah Mansour ambaye alimuelezea majukumu ya msingi ya BoT pamoja na malengo ya kushiriki maonesho ya Nane Nane visiwani, Zanzibar.
Afisa wa Benki Kuu Kauthar Mugheir akimuelekeza mmoja wa wananchi waliotembelea banda la BoT namna bora ya kutambua alama za usalamakatika noti zetu.
Maafisa wa Benki Kuu wakitoa elimu kwa wananchi katika banda la BoT.
Benki Kuu inashiriki katika maonesho ya kilimo ya Saba yenye kauli mbiu ‘Kilimo ni utajiri, kila mtu atalima’ yanayoendelea, na inatoa wito kwa wananchi kufika katika banda lao ili kujipatia elimu ya majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania.