Mkaguzi wa dawa mwandamizi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kanda ya Kati jijini Dodoma Benedict Brashi ametoa wito kwa wananchi kuwa makini juu ya matumizi na namna sahihi ya utunzaji wa dawa wakati akizungumza katika maonesho ya kitaifa ya wakulima (Nanenane) yanayoendelea mkoani Dodoma.
Akieleza namna ya utumiaji sahihi wa dawa Bw. Benedict Brashi amesema kuwa wananchi ni lazima wafahamu namna sahihi ya utumiaji wa dawa na utunzaji sahihi wa dawa ili kuepukana na kurujirudia kwa magonjwa Mara kwa Mara hapa ni muhimu kumaliza dozi kwa usahihi na kwa muda muafaka.
Amesema kuwa”wagonjwa wengi wanashindwa kumaliza dozi kwa wakati na hivyo kupata magonjwa sugu yanayosababisha matatizo makubwa kiafya, Kunawengine wanapata dozi hospitalini lakini inafika mahali hizo dawa alizopewa hazitumii na kuna wengine wanagawana lakini wananchi lazima waelewe kuwa ukipewa dozi ni ya mtu mmoja.
Hata hivyo tumekuja hapa kwenye maonesho ya Nanenane kwa ajili ya kuwapa elimu wananchi kuwa wawe waangalifu na kusoma aina ya dawa zinapotolewa kabla ya kunza kutumia.
kuna dawa ambazo zimethibitishwa na serikali ni sahihi kabisa kwa matumizi, wananchi wanapaswa wafahamu hilo ili kusudi kuwepo na usalama zaidi.
Ameongeza kuwa kuwasaidia wananchi namna ya utumiaji wa dawa ni jukumu letu sisi kama TMDA
Bw. Benedict amesema baadhi ya wananchi wanaojihusisha na utengenezaji wa dawa binafsi wahakikishe zinapitia na kufanyiwa ukaguzi maalumu ili kusudi zithibitishwe na serikali waweze kuuza kwa urahisi.
Jambo muhimu hapa ni kuwa dawa hizo zinatakiwa zichunguzwe kwa usahihi na tukishachunguza tujue na kuona zinaleta matokeo yaliyotarajiwa kwa jamii.