Bodi ya Bima ya Amana (DIB) imesema mpango wake wa miaka mitano wameweka mkakati wa kutoa elimu kwa umma mpaka kufikia 2026/2027 wawe wamewafikia wateja wa benki kwa asilimia 30 na umma wa watanzania asilimia 20.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo Meneja Uendeshaji DIB Nkano Magina amesema wapo kwenye maonesho hayo ili kutoa elimu kwa wananchi ambapo wamejipanga kuhakikisha elimu hiyo inatolewa kwa kila mwananchi.
Amesema katika mpango huo DIB itatumia majukwaa mbalimbali kuwafuata wananchi katika maeneo mbalimbali kama masoko, shuleni na mikusanyiko mbalimbali kama vile makongamano na mikutano
Ameongeza kuwa pia watatumia vyema vyombo vya habari yakiwemo magazeti, Runinga, Redio na mitandao ya kijamii ukizingatia kwamba kwa sasa dunia iko kiganjani kwa hiyo tutakapotumia vizuri mitandao ya kijamii maana yake tutawafikishia taarifa wananchi kiganjani mwao
“DIB inawakaribisha wananchi mbalimbali kwenye banda lao kupata elimu ya usalama wa fedha zao walizoweka benki kama akiba”,Amesema.