Katibu wa Kamati ya Wataalam Ofisi ya Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Mohamed Baruani (kushoto), akimpa maelezo kuhusu moja ya vitabu, mmoja wa waumini wa dini ya kiislamu aliyetembelea banda la BAKWATA, leo katika maonesho ya Nane nane, Nyamhongolo, Manispaa ya Ilemela.
Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke, akiwaonesha baadhi ya wananchi moja ya vitabu vya dini vinavyopatikana katika Banda la BAKWATA, leo katika maonesho ya Nane Nane.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu na wananchi waliotembelea banda la BAKWATA, leo wakionesha vitabu vya dini hiyo katika maonesho ya Nane Nane.Wa pili kutoka kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Alhaji Hasani kabeke.
Sheikh Othman Masasi,leo akionesha eneo la litakalotumiwa na waumini wa kiislamu kwa ajili ya ibada ya swala mbalimbali lililopo nyuma ya banda la BAKWATA,katika maonesho ya Nane Nane, Nyamhongolo.
………
NA BALTAZAR MSHAKA, ILEMELA
WATANZANIA wameaswakuchngamkia fursa, kuthamini na kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na sekta zaserikali kupitia Maonesho ya Wakulima (Nane Nane) ili kuona nchi ilipofikiakiuchumi,kijamii na kiimani.
Sheikh wa Mkoawa Mwanza, Alhaji Hasani Kabeke,amesema leo katika Maonesho ya Nanenaneyanayofanyika katika eneo la Nyamhongolo,katika Manispaa ya Ilemela.
Amesema Maoneshoya Nane Nane yanayofanyika jijini Mwanza,ni fursa kwa wananchi wa imani na dini mbalimbali na si ya wakulimana wafugaji pekee,hivyo wayathamini kwa kutembelea mabanda wakajifunze na kuonanchi yetu ilipofikia kiuchumi, kijamii na kiimani.
Sheikh Kabeke amesema kutokana na fursa zilizopo serikali yaawamu ya sita,katika maonesho ya mwaka huu, imetoa fursa kwa taasisi za dini kuoneshakazi zinazofanyika katika jamii, hivyo ni fursa kwa wananchi kutembelea mabandahayo wajifunze na kupata elimu ya mambo mbalimbali.
“Wananchi wamikoa ya Kanda ya Ziwa wanaopata fursa ya kufika Nyamhongolo,watembelee mabandayote yakiwemo ya dini,wazione fursa na wajifunze na kupata elimu ya masualambalimbali ya kiuchumi,kijamii na kiimani,”amesema.
Sheikh Kabeke amewasisitizakuwa wakitembelea mabanda yote wataona mambo makubwa yanayofanyika katika jamii,mbalina elimu wataziona fursa nyingi zinazoweza kuwasaidia baadaye.
Kiongozi huyowa kiroho amewakumbusha Watanzania kuendelea kudumisha amani na utulivu ulioponchini tunapoelekea katika uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa serikali za mitaa.
“Niwasihituendelee kulinda amani na utulivu wa nchi yetu, hata maonesho haya ya NaneNane yanayofanyika ni ushahidi wa utulivu mkubwa uliopo,hivyo tukiudumisha tutaonafaida za utulivu huo,”amesema