Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) Dkt. Thomas Bwana amewakaribisha Wakulima na wadau mbalimbali kutembelea eneo la TARI katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa (Nanenane) ili kujifunza teknolojia Bora za Kilimo zilizofanyiwa Utafiti katika mnyororo wa thamani.
TARI inashiriki maonesho ya Nanenane kitaifa Nzuguni Dodoma pia katika Kanda zingine za maonesho haya ambayo ni muhimu kwa Wakulima na wadau wa Kilimo kupata elimu na maarifa sahihi kutoka kwa Wataalamu juu ya kanuni Bora za Kilimo na fursa za Kilimo.
Mwezi Julai ya mwaka huu- 2024, TARI imetoa Mbegu mpya aina 16 za Mazao ya Maharage, Karanga na Korosho zilizoidhinishwa na kamati ya taifa ya Mbegu. Mbegu hizo zina sifa za ziada kulinganisha na mbegu ambazo Wakulima wamekuwa wakizitumia na elimu kuhusu mbegu hizo ni Miongoni mwa mengi yanayopatikana katika Banda la TARI kwenye maonesho haya.
Maonesho ya Nanenane mwaka huu, yana kaulimbiu ya Chagua viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.