Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Kampeni ya Tutunzane Mvomero mkoani Morogoro tarehe 03 Agosti, 2024. Kampeni hiyo ina lengo na kuepusha migogoro ya Wakulima na wafugaji pamoja na watumiaji wengine wa ardhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiangalia jinsi mfanyabiashara alivyohifadhi nyama ya ng’ombe ambayo anaiuza ndani na nje ya nchi, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Tutunzane, Mvomero mkoani Morogoro tarehe 03 Agosti, 2024.
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wakiwa kwenye Uwanja wa Sokoine Mvomero kwa ajili ya Kampeni ya Tutunzane Wilayani humo Mkoani Morogoro tarehe 03 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Akiwa kwenye picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa kiwanda cha Sukari Mtibwa, leo tarehe 3 Agosti, 2024.