NA MWANDISHI WETU, DODOMA
Mfuko
wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unawaalika wananchama na
wananchi kutembelea banda la Mfuko huo katika Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na
Wavuvi (Nane Nane) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika katika iwanja
vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Kanda
ya Nyanda za Juu Kusini inajumuisha Mikoa ya Iringa, Njombe, Songea, Mbeya, Songwe, Rukwa
na Katavi.
Akizungumzia
ushiriki wa PSSSF kwenye Maonesho hayo, Kiongozi wa banda PSSSF, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bw. Edward
Kyando, amesema, Mfuko huo unawahudumia Watumishi wa Umma, ambao nao ni
washiriki katika Maonesho hayo wakiwakilisha taasisi zao.
“Lakini
si tu watumishi ambao ni wanachama wetu, pia kuna fursa mbalimbali za kiuchumi
kupitia uwekezaji wa Mfuko kwenye maeneo ya viwanda, lakini pia majengo na nyumba
za makazi, hivyo wananchi nao wanakaribishwa kupata taarifa za fursa
zinazopatikana PSSSF.” Amesema.
Kwa
wananchama watakaotembelea banda la PSSSF watapata taarifa mbalimbali
zinazohusiana na uanachama wao kama vile, Taarifa za Michango, Taarifa za
Mafao, Taarifa za Uwekezaji na pia wanachama wataelimishwa jinsi ya kupata huduma
kupitia mtandao maarufu PSSSF Kidijitali.
“Huduma
hii ya PSSSF Kidijitali, inamuwezesha Mwanachama kujihudumia mwenyewe kupitia
simu janja kupitia, atapata huduma zote ikiwa ni pamoja na kuwasilisha madai
mbalimbali. Halikadhalika kwa wastaafu nao wanaweza kujihakiki.” Alifafanua.
Kauli
Mbiu ya Maonesho ya mwaka huu ni “Chagua
Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na
Uvuvi”.
Afisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi
wa Umma (PSSSF), Bw. Emilyo Mwakalobo (kushoto), akimuhudumia mwanachama wa
Mfuko huo aliyetembelea Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane)
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika katika iwanja vya John Mwakangale
jijini Mbeya.
Afisa
wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Edward Nzota
(kushoto), akimuelekeza mwanachama wa Mfuko huo jinsi ya kutumia PSSSF
Kidijitali kupitia simu yake mkononi (simu janja) kwenye banda la PSSSF kwenye
Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane) Kanda ya Nyanda za Juu
Kusini yanayofanyika katika iwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Edward Nzota (kulia) Mfanyakazi wa PSSSF, akifurahia jambo na Mwanachama wa Mfuko huo aliyefika kuhudumiwa
Timu
ya Maafisa wa PSSSF ikiwa tayari kuwahudumia wanachama na wananchi katika
viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya. Kutoka kushoto kwenda kulia ni Edward
Nzota, Emilyo Mwakalobo, Swinford Mndellah, Joyce Mtinangi na Edward Kyando.
Mwanachama,
akizungumza mbele ya wafanyakazi wa PSSSF alipotembelea banda la Mfuko huo
kuhudumiwa
Timu ya PSSSF Nanenane 2024 Kanda’s