Wananchi wameendelea kujitokeza katika Maonesho ya Wakulima kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma.
Pichani wataalamu wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Bw. Romuli Mtui na Beatrice Kallanga, wakitoa maelezo ya kazi za DIB kwa wananchi waliotembelea banda lao.
Kazi kubwa ya Bodi ya Bima ya Amana ni kuwalinda wenye amana dhidi ya upotevu wa amana zao pale ambapo benki au taasisi zao za fedha zinaposhindwa kufanya kazi au zinapofilisika.
Pamoja na kazi hiyo, DIB inatathmini na kukusanya malipo ya bima au michango kutoka katika benki na taasisi za fedha, kusimamia mfuko wa Bima ya Amana, kuwalipa wenye amana fedha zao iwapo benki au taasisi ya fedha itashindwa kuendelea kazi au ikifilisika.
Bodi ya Bima ya Amani pia inafanya ufilisi wa benki au taasisi za fedha zilizoshindwa kufanya kazi au kufilisika pale inapoteuliwa na Benki Kuu ya Tanzania kufanya hivyo.