Meneja wa PSSSF mkoa wa Dodoma,Bwana Michael Bujiba akiangalia bidhaa ya viatu katika babda hilo wakati alipotembelea maonesho ya Nanenane eneo la Nzuguni jijini Dodoma.
…………..
*Yatangaza Huduma za Kidigitali
Dodoma, Tarehe 2 Agosti 2024
Maonesho ya wakulima nanenane yanafanyika kitaifa jijini Dodoma huku taasisi mbalimbali zikitumia fursa kutoa elimu na huduma kwa wananchi.
Miongoni mwa washiriki wakubwa ni Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Akiwa katika banda la PSSSF Meneja wa PSSSF mkoa wa Dodoma,Bwana Michael Bujiba amesisitiza dhamira ya Mfuko huo katika kutoa huduma bora kwa wanachama.
“Kupitia teknolojia ya kidigitali, sasa wanachama wanaweza kuwasilisha madai yao ya mafao kwa njia rahisi na haraka zaidi,” alisema Bwana Bujiba. “Huduma hizi zitawasaidia wanachama kuwasilisha madai yao popote walipo bila kufika ofisini.”
Wanachama wamepokea kwa furaha taarifa hizi na kuonesha shukrani zao kwa PSSSF kwa kuboresha huduma zao. Teknolojia ya kidigitali imeonekana kuwa mkombozi kwa wastaafu pia, kwa kuwapatia fursa ya kujihakiki kwa urahisi.
Maonesho ya nanenane yanawakilisha jitihada za PSSSF katika kuelimisha umma kuhusu huduma mbalimbali zinazotelewa na Mfuko huo.
PSSSF inashiriki katika maonesho ya nanenane jijini Dodoma katika viwanja vya Nzuguni, Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale na Zanzibar katika viwanja vya Dole, Kizimbani.
Meneja wa PSSSF mkoa wa Dodoma,Bwana Michael Bujiba akipata maelezo kutoka kwa maafisa wa PSSSF Salvatory Rugumisa na Violent Michael wakati alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Nanenane eneo la Nzuguni jijini Dodoma.