Katibu Mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe akiwasalimia wafanya kazi wa shirika la Bima NIC wakati alipotembelea mabanda mbalimbali leo Agosti 2, 2024 katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma
Agosti 2, 2024 na Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika la NIC ,Karim Meshack akizungmza na waandishi wa habari katika banda la shirika hilo.
………………….
Shirika la Bima (NIC) linatoa elimu kwa wakulima ili waweze kujua na kutambua thamani ya kukata bima hatua itakayosaidia kujikinga na majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri uzalishaji wao.
Hayo yamebainishwa Leo Agosti 2, 2024 na Mkurugenzi wa Masoko wa Shirika hilo,Karim Meshack wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea kufanyika Nzuguni Jijini Dodoma.
Amesema NIC ni Kampuni kiongozi kwenye sekta ya bima hivyo ni lazima wafanye utafiti ili wajue changamoto zinazowakabili wakulima wakati wa kulima,kuvuna na kabla ya kukuza mazao yao.
“Changamoto ambazo zinatokea wakati wa kulima zinazoweza kuathiri kilimo ni wanyama wakali kuvamia mashamba,mvua nyingi zinazozidi uwezo wa mimea kustahimili pamoja na masuala ya ukame,kwahiyo tukatengeza bidhaa ya bima ambayo inajibu changamoto hizo ambazo ni bima ya kilimo na mifugo na ni mahususi kwa wakulima hasa kuwaelewesha katika maonesho haya ya wakulima”,amesema Meshack
Amesema lengo la bima ni kumrejesha mbima pale alipokuwa mwanzo kabla ya kupata majanga huku akiongeza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuwa na bima hususani kwenye kilimo.
“Ukiwekeza milioni 500 kwenye kilimo ukapata majanga sisi kama Bima tutarejesha fedha zako zote na utaendelea na maisha yako bila kuwa na changamoto yoyote”, amesema
Mwisho ameeleza kuwa Kilimo ndio uti wa mgongo na ni chachu ya kukua kwa uchumi wa nchi.