Maafisa Majenerali Wastaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Gabriel Sauli Mhidze, Meja Jenerali Charles Mang’era Mbuge, Meja Jenerali Ally Mzee Katimbe, Meja Jenerali Chelestino Elias Msolla, Brigedia Jenerali William Stephene Likangaga pamoja na Brigedia Jenerali Andrew Elinipenda Mughamba wakitoa heshima ya katika hafla ya kuagwa iliyofanyika leo Agosti 2, 2024 katika Viwanja vya Twalipo, Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda akipiga saluti akiwa katika hafla ya kuwaaga Maafisa Majenerali Wastaafu sita wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyofanyika leo Agosti 2, 2024 katika Viwanja vya Twalipo, Dar es Salaam.
Maafisa Majenerali Wastaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Jenerali Gabriel Sauli Mhidze, Meja Jenerali Charles Mang’era Mbuge, Meja Jenerali Ally Mzee Katimbe, Meja Jenerali Chelestino Elias Msolla, Brigedia Jenerali William Stephene Likangaga pamoja na Brigedia Jenerali Andrew Elinipenda Mughamba wakikagua gwaride maalumu kwa ajili ya kuwaaga lilifanyika leo Agosti 2, 2024 katika Viwanja vya Twalipo, Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda (kulia) akimkabidhi ufungua wa gari mpya Meja Jenerali Mstaafu Charles Mang’era Mbuge (pichani) pam0ja na Majenerali waastafu wengine wa JWTZ.
Gwaride rasmi la kuwaaga Maafisa Majenerali Wastaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likipita mbele ya jukwaa kuu kutoa heshima.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Jenerali Wastaafu Meja Jenerali Gabriel Sauli Mhidze, Meja Jenerali Charles Mang’era Mbuge, Meja Jenerali Ally Mzee Katimbe, Meja Jenerali Chelestino Elias Msolla, Brigedia Jenerali William Stephene Likangaga, Brigedia Jenerali Andrew Elinipenda Mughamba.
Picha za matukio mbalimbali (Picha na Noel Rukanuga)
…..
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limefanya Gwaride rasmi la kuwaaga Maafisa Jenerali Wastaafu sita ambao wametimiza umri wa lazima wa kustaafu, huku Maafisa hao wakitoa wito kwa jeshi kuendelea kufanya kazi kwa uweledi.
Akizungumza leo Agusti 2, 2024 jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwaaga Maafisa Jenerali Wastaafu sita iliyofanyika katika viwanjwa vya Twalipo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda, amesema kuwa utaratibu wa kuwaaga maafisa wastaafu ngazi ya Jenerali ni sehemu ya utamaduni wao.
Jenerali Mkunda amesema kuwa wanatambua mchango wao mkubwa wa maafisa majenerali wastaafu, huku akieleza kuwa bado wataendelea kuwatumia jeshini kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mujibu wa sheria.
“Utaratibu huu wa kuwaaga unaonesha ni mwisho wa wtumishi wao jeshini na baada ya tukio hilo watakabidhiwa vitambulisho vyao vya kustaafu, lakini wataendelea kuwa sehemu ya jeshi katika kipindi cha miaka mitatu kwa mujibu wa sheria na baada ya miaka hiyo kumalizika inatakuwa hiari yao kulitumika Jeshi” amesema Jenerali Mkunda.
Akizungumza kwa niaba ya Maafisa Jenerali Wastaafu sita , Meja Jenerali Mstaafu Gabriel Sauli Mhidze, amesema kuwa leo ni siku yake ya furaha baada ya kulitumikia Jeshi miaka 41 kwa nidhamu pamoja na uweledi mkubwa.
Maafisa Jenerali Wastaafu sita walioagwa leo ni Meja Jenerali Gabriel Sauli Mhidze, Meja Jenerali Charles Mang’era Mbuge, Meja Jenerali Ally Mzee Katimbe, Meja Jenerali Chelestino Elias Msolla, Brigedia Jenerali William Stephene Likangaga pamoja na Brigedia Jenerali Andrew Elinipenda Mughamba.