Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Godfrey Mnzava ameuwasha Mwenge wa Asili wa Mwitongo wilayani Butiama Mkoani Mara ikiwa nitukio ambalo limekuwa likifanyika Miaka yote ambapo mwaka huu tukio hilo limekuwa lakitofauti kutoka na uwepo wa maadhimisho ya Miaka 60 ya Mwenge wa Asili wa Mwitongo
Akizungumzia mara baada ya Kutekeleza Jambo hilo kiongozi Huyo wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa amesema kuuwasha Mwenge wa Asili wa Mwitongo nakutembelea kaburi la Baba wa Taifa nikupata baraka katika mbio hizo ambazo wanaendelea nazo hadi Oktoba 14 utakapozimwa Mkoani Mwanza.
“Tumekuja Kupata baraka kwa Muasisi wa Mwenge wa Uhuru ambae alisistiza kupinga vitendo vya Rushwa madawa ya kulevya ambapo pia alisistiza utunzaji wa Mazingira jambo ambalo limekuwa likitekelezwa na viongozi wengine”Alisema Mnzava kiongozi Mwenge wa uhuru kitaifa 2024.
Katika hatua nyingine alisema mwenge wa Uhuru anasisistiza wananchi kujitokeza kushiriki Uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Amani ikiwa nitunu kubwa iliyoachwa na Hayati Mwalimu Julius kambarage nyerere
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi ameshiriki maadhimisho ya miaka 60 ya Mwenge wa Mwitongo nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuwataka watanzania kumkumbuka Mwalimu Nyerere kwa kuyaenzi mazuri yote aliyoyasimamia katika uhai wake