Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amekerwa na hujuma zinazofanyika na baadhi ya viongozi dhidi ya miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya kata ya Kiseke
Hayo yamebainishwa wakati wa ziara ya mbunge huyo akikagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Jimbo lake ambapo akiwa viwanja vya Kabambo kata ya Kiseke alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata hiyo akafafanua kuwa ipo miradi inayotekelezwa ikiwa chini ya kiwango kama jengo jipya la wodi ya Zahanati ya Luhanga ambalo limetumia mifuko mingi ya saruji likiwa sio imara pamoja na barabara ya mlima wa rada ambayo baadhi ya mifuko ya saruji ilipotea bila kujulikana kipindi Cha ujenzi
‘.. Kwa kuangalia tu hapa inaonekana ni mchanga pekee umetumika bila saruji na kama imetumika basi ni kidogo sana, Hapa tumeleta mifuko 100 na tofali 3800 lakini hakuna kilichojengwa, Inauma sana ukizingatia wakati mwengine hatutoi fedha za Serikali ni Mbunge na Wadau wake anaamua kuunga mkono juhudi za wananchi ..’ Alisema
Aidha Mhe Dkt Mabula amemshukuru Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan kwa fedha za miradi ya maendeleo huku akiwaasa wenyeviti wa Serikali za mitaa kata ya Kiseke kuendelea kushirikiana na kusimamia fedha za miradi ya maendeleo zinazoletwa katika maeneo yao
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Kabambo Ndugu Maulid Aungu mbali na kumshukuru Mbunge huyo kwa jitihada zake za kusukuma maendeleo ameongeza kuwa kata yao imekosa kiongozi mzuri wa kuwaunganisha hivyo kusababisha kusuasua kwa shughuli za maendeleo pamoja na ujenzi wa chini ya kiwango wa miradi kwakuwa hakuna usimamizi mzuri
Suzana Clemence ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake ya CCM (UWT) kata ya Kiseke ambapo amempomshukuru Mbunge Dkt Mabula kwa juhudi zake katika kutatua kero mbalimbali za kata hiyo na kwamba chama Cha Mapinduzi kinamuamini na kinamuunga mkono kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi
Asteria Kihangwa ni mwananchi wa mtaa wa Kabambo ambapo amelalamikia unyang’anyi wa maeneo yao ya asili unaofanywa na baadhi ya viongozi wasiokuwa waadirifu huku Joseph Ngoji akilalamikia ucheleweshaji wa fidia katika eneo lake lililotwaliwa na manispaa Kwa utekelezaji wa shughuli za umma sanjari na changamoto ya upatikanaji wa Maji safi na salama