Mwita Patrick Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania BoT akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la BoT ili kupata elimu ya fedha kwenye banda la BoT katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.
…………….
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imelenga mfumuko wa bei ubaki katika lengo la kati la asilimia tatu na tano kwa mwaka 2024/25
Hayo yamebainishwa Leo Agosti 2, 2024 na Mwita Patrick Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania BoT wakati alipokuwa akizungumza kwenye banda la Benki hiyo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni Jijini Dodoma.
Amesema jukumu la BoT ni kuhakikisha kiwango cha fedha kwenye mzunguko kinakuwa kipo sawia na malengo mapana ya kiuchumi.
“Mwaka huu tuna makadirio ya ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.4 ambapo mwaka jana uchumi ulikuwa kwa asilimia 5.1, Sera ya fedha ina jukumu la kuhakikisha fedha zilizoko kwenye mzunguko zinachangia kufikia haya malengo ya kuwa na mfumuko wa bei ambao uko ndani ya wigo wa asilimia 3 na 5”, amesema.
Kiwango cha fedha katika mzunguko wa Uchumi lazima kiwiane na mahitaji ya shughuli za kiuchumi Ili kuhakikisha malengo ya mfumuko wa bei na lengo la ukuaji wa Uchumi linafikiwa. Na endopo kiwango hicho cha fedha kikizidi Benki KUU kupitia nyenzo mbalimbali za sera ya fedha hukiondoa kwenye mzunguko, hivyo hivyo kikipungua pia Benki KUU kupitia nyenzo hizo hizo za sera ya fedha hukiongeza katika mzunguko wa kiuchumi’
“Benki Kuu inatumia nyenzo mbalimbali za sera ya fedha ili kuhakikisha kuwa lengo la uendeshaji linaendana na riba ya benki Kuu ambapo nyenzo Kuu za utekelezaji wa sera ya fedha ni pamoja na Benki Kuu kuingia mikataba ya mauziano au manunuzi ya dhamana za muda mfupi na benki za biashara. Nyenzo nyingine ni uuzaji na ununuzi wa dhamana za serikali na uuzaji na ununuzi wa fedha za kigeni katika soko la jumla la fedha za kigeni baina ya mabenki.
Benki Kuu ya Tanzania hutumia nyenzo mbalimbali za sera ya fedha ili kuhakikisha kuwa lengo la uendashaji linaendana na riba ya Benki Kuu. Aidha, kupitia nyenzo hizi, Benki Kuu hubadili ujazi wa fedha na gharama za mikopo katika uchumi.
Nyenzo za msingi hujumuisha Benki kuu kuingia mikataba ya mauziano au manunuzi ya dhamana za muda mfupi na benki za biashara (repurchase agreement and reverse repurchase agreement) ili kuhakikisha kuwa kiwango cha ukwasi kinakuwa chenye kuridhisha.
Nyenzo zingine ni pamoja na uuzaji na ununuzi wa dhamana (Debt Securities), na uuzaji na ununuzi wa fedha za kigeni katika soko la jumla la fedha za kigeni baina ya mabenki.
Pia kiwango cha amana za benki za biashara kinachotakiwa kuwekwa kisheria Benki Kuu (Statutory Minimum Reserve) na riba inayotumika kutoza benki za bishara au Serikali zinapochukua mikopo Benki kuu hutumika kama nyenzo za sera ya fedha. Pamoja na nyenzo hizo, Benki kuu pia hutoa mikopo ya muda mfupi ambayo hutakiwa kurudishwa ndani ya siku husika na ile ya siku moja (Intraday and Lombard loan facilities).Vilevile, Benki Kuu inaweza kutumia nyenzo nyingine za sera ya fedha kuendana na mahitaji.
Aidha, amesema wana majukumu mbalimbali katika utendaji wao wa kazi ikiwemo kutoa takwimu za kiuchumi,wanafanya tafiti za masuala ya fedha na uchumi pamoja na kuandaa ripoti mbalimbali za kiuchumi.
Meneja Mawasiliano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT Bi. Vick Msina akimkabidhi zawadi mmoja wa wananchi waliotembelea katika banda la Benki hiyo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo Agosti 2, 2024.
Meneja Mawasiliano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT Bi. Vick Msina pamoja na Mariam Kopwe kutoka Benki Kuu ya Tanzania BoT wakiwa kwenye banda la Benki hiyo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma leo Agosti 2, 2024.
Marwa Patrick Mchumi kutoka Benki Kuu ya Tanzania BoT akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la BoT ili kupata elimu ya fedha kwenye banda la BoT katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.
Geofrey Jonas Valonge Afisa wa Benki Kuu BoT kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki kushoto na Francis Mdoe Afisa wa Benki Idara ya Huduma za Kibenki BoT Dodoma wakiwaonesha noti halisi na noti bandia baadhi ya wananchi waliotembelea banda hilo.
Geofrey Jonas Valonge Afisa wa Benki Kuu BoT kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki kushoto na Francis Mdoe Afisa wa Benki Idara ya Huduma za Kibenki tawi la BoT Dodoma kulia wakiwasikiliza baadhi ya wananchi waliotembelea banda hilo.