Na Mwamvua Mwinyi, Mafia – PWANI
Agosti 1,2024
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Pwani, Mhe. Subira Mgalu amegawa mashuka ishirini (20) katika hospitali ya Wilaya ya Mafia, katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika sekta ya afya wilayani humo.
Mashuka hayo, ni kati ya mashuka 100 ambayo Wabunge wote wanawake kila mmoja amepewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kutolewa katika maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za afya nchini.
Aidha, Mhe. Mgalu ametembelea hospitali hiyo na kukagua majengo la ICU, na Emergency ambayo Serikali imegharamia takribani shilingi Milioni mia tisa katika ujenzi wake.
Ameeleza Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kusogeza huduma bora na kuongeza majengo katika sekta ya afya.
“Tunamshukuru Rais kwa jitihada zake za kutekeleza ilani katika sekta ya afya ,tumuunge mkono na kuendelea kumuombea ili aendelee kufanya makubwa kuinua uchumi na maendeleo nchini”